ATHARI ZA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
Pale
mtu anapoangalia picha za ngono pole pole ataanza kuzoea na kupendelea mitindo
na mambo yanayofanywa katika picha hizo na hata mambo ambayo alikuwa hayapendi
atajikuta ameanza kuyapenda. Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kuna watu ambao
baada ya kuzoea picha za kawaida wakajikuta wameanza kutamani kufanya mapenzi
na wanyama. Mimi mwenyewe nimeshuhudia hilo baada ya mama mmoja kunipigia simu
kuwa mume wake ameanza kufanya mapenzi na wanyama. Hivyo inatokana na kwamba pale
mtu anapoangalia kitu kwa muda mrefu inafikia hatua akili yake inakiona kama
kitu cha kawaida kwa kuwa walizoe msisimko mkubwa wa mwanzonii na sasa msisimko
h uo unakuwa umepungua baada ya kuangalia picha hizo kwa muda fulani.
Hatari
kubwa kwa watumiaji wa picha za ngono ni kujikuta wamepoteza hamu ya tendo la
ndoa katika hali ya kawaida. Jambo lingine ni kuiga mambo ambayo ni machafu
sana kwa kuwa katika picha hizo unaona watu wanaonekana kufurahia mambo hayo
machafu. Kwa mfano, kesi ya watu kutaka kufanya mapenzi kinyume na maumbile
imeongezeka sana kwa wanaume na wanawake. Mbaya zaidi kwa mtu alieangalia picha
hizo kwa muda mrefu atapata shida kuendelea kuvutiwa na muonakano wa mpenzi
alie nae kwa muda mrefu. Kwa maneno mengine itafikia hatua anamuona mke au mume
wake anaboa. Utafiti uliofuatilia ndoa 200 toka 2006 hadi 2012 ulithibitisha
kuwa katika ndoa ambapo mwanaume anaangalia picha za ngono mara 1 au zaidi kwa
siku zinakuwa na migogoro mingi zikilinganishwa na zile zisizokuwa na tatizo
hilo. Katika ndoa zenye tatizo hilo kosa dogo lilileta migogoro mikubwa,
kulaumiana kwingi, kutoelewana kwingi na
kuleta makosa ya zamani kumkandamiza mwingine.
Mwanamke
au mwanaume anaeangalia picha hizo za ngono atalinganisha mambo anayofanyiwa na
mke wake na yale anayoyaona katika picha hizo na lazima mpenzi wake ataonekana
kuwa na mapungufu katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mitindo anayotumia,
ukubwa au upana na urefu wa maumbile, nguvu au kasi ya utendaji na utundu
mwingine katika kucheza ngoma ya wakubwa. Kwa kuwa lazima mmoja ataonekana na
mapungufu na yule anaeona mapungufu hayo atakosa ujasiri wa kumuambia mwenzie
na hivyo mvuto na hisia kupungua. Hisia zinapopungua na hali hiyo kujirudia
rudia chuki inaanza kurudi kwa pole pole na penzi kunyauka. Ukweli wa jambo
hilo ulionekana katika utafiti miongoni mwa makahaba ambapo asilimia 80 ya
makahaba walishuhudia wateja wao kuwaonyesha mitindo toka kwenye picha za
ngono, mitindo ambayo wateja hao walitaka kuitumia katika kucheza ngoma ya
wakubwa na makahaba hao.
Watu
wanaoiga mambo wanayoyaona kwenye picha za ngono hawajui kuwa wengi wa wahusika
wamelazimishwa kushiriki picha hizo, na haikuwa hiyari yao kufanya hivyo.
Kutokana na kutokujua hilo wengine wanashangaa kuona wapenzi hawapo tayari
kujaribu mambo mapya yanayopendekezwa na wapenzi wao na hivyo kuleta mvutano
kati yao. Kutokana na hali hiyo tafiti nyingi zimeonyesha wazi kuwa watu
walioangalia picha za ngono ndoa zao zinakosa furaha na nyingine kuvunjika.
Naweza kusema kuwa kuvunjika kwingi kwa mahusiano kabla ya ndoa yanasababishwa
na hali hiyo.
Mbaya
zaidi kuliko zote ni kwamba uangaliaji wa picha za ngono kunachangia katika
kupunguza nguvu za kiume kwa wanaume wengi, na kwa wanawake zinachangia
kupunguza hamu ya tendo la ndoa. Mtu anapokumbatiwa, kupigwa mabusu mengi au
kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine kuna kiasi fulani cha kichocheo cha DOPAMINE kinacho miminwa kwenye ubongo
kupitia mzunguko wa damu na kumfanya mtu afurahie tendo la ndoa. Ila kiasi
hicho kikizidi kipimo alichopanga muumbaji wetu inasababisha matatizo . Mtu
anapoangalia picha za ngono yanatokea mafuriko ya kichocheo hicho cha DOPAMINE na inasababisha vipokeaji vya
hisia katika mishipa ya fahamu (Receptors) kushindwa kufanya kazi na kuwa butu.
Japokuwa ubongo utaendelea kuleta kichocheo cha hisia tamu cha DOPAMINE mtu anashindwa kupata msisimko
na hivyo kushindwa kuwa na nguvu za kiume za kutosha, na kwa mwanamke kutokuwa
na hisia hata mwanaume ajitahidi vipi kumwandaa.
Hapo unaweza kuona jinsi ndoa
inavyoweza kuvunjika, mwanaume hana nguvu za kutosha na mwanamke ana hamu
lakini mwanaume hana ujanja, inaleta mvutano. Au kwa upande mwingine mwanaume
ana nguvu na hamu lakini mwanamke hana hamu au hajisikii raha yoyote na
atalichukia tendon a kuleta migogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni