DALILI
ZA MPENZI ALIEBOREKA NA WEWE
Mahusiano mengi sana
yapo katika hali ya kusikitisha, na wengi hawajui wamefikaje fikaje katika hali
hiyo jambo ambalo linatisha. Unapokutana na hali ambayo hujui jinsi ya
kuiondoa, inatisha sana na ni sawa sawa na mtu ambae ameanguka kwenye dimbwi
refu la kuogelea wakati huo na yeye hajui kabisa kuogelea. Jambo la ajabu
katika mahusiano mengi ya kimapenzi ni kwamba mtu anaweza kuwa ameboreka na
mpenzi wake lakini hajui afanye nini kubadili hali hiyo mbaya, na mbaya zaidi
akashindwa hata kutafuta njia za kuibadili hali hiyo. Ukijua kuwa mpenzi wako
ameboreka unaweza kuanza kutafuta njia za kumsaidia achangamke lakini usipojua
hilo na ukaendelea kama vile hakuna tatizo unakaribisha majanga katika uhusiano
wenu.Matokeo hayo nayaona pale mteja anaponiambia kuwa mpenzi wake
kabadilika na sababu haijui na anaumia
kwa kuwa anampenda sana.
Unapohisi kuwa mpenzi wako ameboreka
upo uwezekano mkubwa kuwa ni kweli
ameboreka na haijalishi kama kosa ni lako au la kwake au mchanganyiko wa yote
ya kwako au yak wake hiyo ni hali ambayo inahitaji ufumbuzi haraka.
Zifuatazo
ni dalili kuwa mpenzi wako ameboreka na wewe au na uhusiano wenu kwa ujumla:
1) Pamoja na bidii yako kubwa bado mpenzi
wako anaonekana kama akili yake ipo sehemu nyingine ofauti kabisa. Katika mazingira kama haya ndio
unasikia mtu unasema “Mpenzi wangu simuelewi” unampigia simu
hapokei kwa wakati na anachelewa sana kukupigia. Unamtumia SMS nzuri za
kimahaba lakini yeye anajibu kikavukavu tu, ukiuliza kitu basi anatoa majibu
mafupi mafupi au mkato mkato.
2) Mara nyingi anakuwa mzito kukujulisha
nyendo zake au mizunguko yake na pindi ukihoji juu ya mwenendo wake anakuwa mkali.
3) Ameanza kukulinganisha na wanawake au
wanaume wengine bila kujali hisia zako.
4) Hapendelei kukuita kwa majina ya
kimahaba kama baby, honey, mpenzi n.k. Pia hapendelei muongelee juu ya kiwango
cha penzi na ubora wake.
5) Unapokuwa na jambo linalo kuhuzunisha au
kukukosesha raha haangaiki kukufariji. Huzuni yako au maumivu yako hayasumbui
nafsi yake.
6) Uso wake hauonyeshi uchangamfu kama pale
mwanzoni. Uonapo mpenzi wako anapokuwa na wewe uso wake upo kama vile amesikia
mtu alietoa hewa mbaya, tambua kuwa ameboreka na wewe kwa kiasi kikubwa.
7) Uonapo anakasirika sana kwa mambo madogo
madogo na hali hiyo ikawa inajirudia rudia hiyo ni ishara kuwa amekuchoka. Na
iwapo mara kadhaa katika mazingira kama hayo anasema mambo yanayoonyesha
kuachana na wewe hiyo ni haja ya moyo
wake basi tambua kuwa yasipotokea mabadiliko kifo cha uhusiano wenu hakiko mbali.
Mara nyingi hali hiyo huambatana na maneno yanayokatisha tamaa.
8) Anakwepa mada zinazohusu madhaifu au
mapungufu yake. Uonapo kuwa mpenzi wako hapendi mzungumzie kwa kina mambo
yanayoharibu ubora wa uhusiano wenu maana yake haoni sababu yoyote ya kupoteza
muda wake katika kujenga uhusiano wenu, yaani ameishiwa nguvu za kujenga na
kupamba uhusiano wenu.
9) Mpenzi wako anapendelea zaidi kuchati na
marafiki zake kuliko kuongea na wewe muwapo pamoja. Lingine linalofanana na
hilo unakuta mpenzi wako anapendelea zaidi kuangalia TV kuliko kuongea na wewe
muwapo pamoja. Hali hii ikiendelea mtajikuta mnaishi kama vile ni kaka na dada
yake.
10)
Ameanza kutumia maneno makalimakali pale
unaposema bila kujali hisia zako au amekuwa mtu wa kufoka foka na kuguna guna.
11)
Uvaaji wake unakuwa wa hovyo hovyo na
hajali sana kupendeza katika uvaaji wake. Ukiwa na mpenzi kama huyo na ghafla
ukaona ameanza kuvaa vizuri maana yake amepata mchepuko.
12)
Ni mara chache sana mmetoka pamoja kwa
chakula au vinywaji au hapendi muonekane pamoja.
13)
Husikilizwi kikamilifu; Ni kweli hakuna mtu
anaependelea hali ya kubishana bishana lakini kuna wakati hali hiyo inajitokeza
na jinsi mpenzi wako anavyo kabiliana na hali hiyo itakupa picha ya mtu alieboreka
na wewe na hategemei faida yoyote ya majadiliano ya aina yoyote. Pale mpenzi
wako anapoanza kukatisha mazungumzo yenu kwa kusema “Yaishe” au “Kila siku jambo
lile lile tu” au “Sitaki kelele
zako” tambua kuwa umekuwa kero kwake japo hoja yako ni halali kabisa. Kama
vile hakuna mtu ambae anapendelea kula chakula kilichopikwa lakini hakikuiva
hakuna mtu anaefurahia kuona haja yake ya kutoa yote yaliomo moyoni imekatishwa
kwa sababu zisizo halali. Mpenzi anaekupenda atakusikiliza kilio chako bila
kujali ni marudio kwa kuwa anaheshimu hisia zako.
14)
Kaacha mambo yanayokusisimua; Mtu alie
boreka na wewe utamuona ameacha kukupa surprise za hapa na pale na amekuwa
mwepesi wa kuahirisha mambo mliokubaliana.
15)
UCHEZAJI
wa ngoma ya wakubwa umeanza
kupungua; Chakula ambacho kimeanza kuchacha kinagundulika kutokana na
kubadilika kwa ladha yake jambo ambalo linakuondolea hamu ya kula chakula
hicho. Uonapo mpenzi wako amepunguza bidii yake katika kuhakikisha unaridhika
na tendo la ndoa tambua ngoma hiyo imechcha na ameanza kuboreka katika eneo
hilo na pia uonapo analeta visingizio vyenye ulemavu ili kuepuka kucheza na
wewe ngoma ya wakubwa ni dalili ya hatari sana..
Ndugu yangu,usijidanganye kwa kusema
mapenzi ndivyo yalivyo wakati huna raha
na uhusiano uliomo. UPO uwezekano wa
kuleta mabadiliko mazuri kama vile wahenga walivyosema penye nia pana njia.Tafuta njia ya kumsaidia
mpenzi wako aelewe umuhimu wa kufurahiana katika uhusiano uliomo kinyume na
hapo utaishi kama mtumwa kwani hisia zako haziheshemiwi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni