SIFA
ZA MWANAUME ASIYEFAA KWA MWANAMKE
Napata
vilio vingi toka kwa wanaume ambao bado wanawapenda wapenzi wao au wake zao
lakini watu hao wamebadilika na kuwafanyia mambo yanayowaumiza mno. Upende au
usipende kuna vigezo ambavyo mpenzi wako anaangalia na unaposhindwa kutimiza
vigezo hivyo mwanamke ataanza kuleta misukosuko ambayo kwako wewe kama mwanaume
utaona kuwa haina sababu. Hebu fikiria, umempenda mwanamke mrembo na yeye
akakukubali na kuapa kuwa hatakuacha kabisa unadhani kwa maneno hayo hawezi
kukuacha?
Nikupe mfano mmoja, kaka mmoja alipata mchumba ambae
alikuwa mrembo sana na kwa miaka 3 uhusiano ulikuwa mtamu mpaka pale huyo kaka
alipoanza matani na dada mwingine. Yeye aliona ni utani lakini baada ya mchumba
wake kuona mtiririko wa mazungumzo yao kwa SMS alijua kuwa mchumba wake anao
uwezo mkubwa sana wa kumsaliti. Japo alikuwa hajathibitisha kabisa alivunja
uchumba huo, unaweza kupiga kelele na kusema kuwa huyo dada alikosea alitafuta
tu kisingizio. Sikiliza dada ambae baba yake alichepuka na kumletea mama yake
UKIMWI lazima atachukia usaliti hata chembe ndogo tu ya usaliti inamtisha sana.
Vifuatavyo ni vitu au mambo mabaya kwa wanawake:
1. MATANGAZO YA UONGO.
Katika miaka
11 ya utoaji ushauri katika Radio na TV nimekutana na kesi nyingi za wanaume
walioachwa japo bado walikuwa wanawapenda wapenzi wao. Wanaume wengi ni
mabingwa katika kutangazia wanawake kuwa wanawapenda lakini hawajui njia sahihi
za kuwathibitishia hilo. Kaka mmoja alishtuka pale ambapo dada ambae alizoea
kumuita “Mpenzi” au “Honey” ama “Darling” alipobadilisha hayo majina na kuanza kumuita huyo kaka “Wewe”. Nilipomuuliza huyo kaka iwapo amewahi
kumpa zawadi yoyote mpenzi wake aliniambia juu ya misaada aliyoitoa kama
kuharibikiwa na simu ya mpenzi wake kulimlazimisha atoe pesa itengenezwe, kumpa
nauli kwenda misibani na vitu vingine. Nikamwambia hiyo sio zawadi bali ni
msaada. Mwanamke hajali maneno unayotumia kumwambia unampenda bali anataka
umfanyie mambo bila ya kuombwa au kuambiwa, hapo ndio anauona moyo wako wa
kupenda. Ukitoa ahadi zako jitahidi uzitimize na pia jitahidi kuwa nae karibu
pale upatapo nafasi.Unaposhindwa kuwa mtu wa vitendo unaonekana kuwa unacheza mchezo wa kuigiza tu.
2. KUHAMIA KITI CHA NYUMA.
Wanaume wengi
sana huonyesha msisimko wao mwanzoni mwa uhusiano na hawaweki mikakati ya
kudumisha shangwe hizo. Baada ya muda fulani uchangamfu uliokuwepo mwanzoni
unapungua na mawasiliano yanakuwa madogo. Mwanzoni wanaume wanakuwa wawazi kwa
wapenzi wao lakini baadae wanaanza usirisiri na hawataki kuulizwa maswali na
wakiulizwa wanakuwa wakali. Utaonekana mbaya kwa mwanamke pale unapomtegea kuwa
yeye ndio awe wa kwanza kukutafuta ,kukupa zawadi na akakubali kila unapotaka
kucheza nae ngoma ya wakubwa. Kufanya hivyo ni sawa na abiria aliekuwa amekaa
kiti cha mbele ndani ya gari na anahamia kiti cha nyuma. Kwa kuwa mwanamke
anakuwa hajapata sababu za kutosha kwa mabadiliko hayo anajua kuwa umemchoka.
3. KUJIFANYA KIPOFU NA KIZIWI.
Wanaume wengi
hawajajifunza kuwa makini katika mahusiano yao jambo ambalo linawaboa wanawake.
Mwanaume hamsifii uzuri wa mpenzi wake, uvaaji wake na bidii yake katika usafi,
anakuwa kama vile kipofu ambaye haoni hayo yote. Hata Mungu alilalamika juu ya
mambo yanayofanana na hayo: “Sikilizeni
enyi viziwi; tazameni enyi vipofu, mpate kuona. Ni nani alie kipofu kama
mtumishi wangu, au alie kiziwi kama mjumbe wangu nimtumaye? Unaona mambo mengi
lakini huyatii moyoni, masikio yako yapo wazi lakini husikii” (ISAYA 42: 19-20).
Ni muhimu mwanaume ajifunze kumsifia mpenzi wake na
kumshukuru kwa mambo anayofanyiwa. Mwanaume mbaya haoni umuhimu wa kumtamkia
mpenzi wake mara kwa mara kama anampenda.
4. UDEREVA.
Asilimia kubwa
ya wanaume wanapata shida kuelewa kuwa mwanamke nae ni mwanadamu mwenye akili
anaehitaji kusikilizwa. Utakuta mwanaume anataka mambo yaende kama anavyotaka
yeye bila kujali hisia za mwanamke. Na sio hilo tu, bali pia wanaume wengi
wabaya sio wepesi kwa kukubali kosa au kuomba radhi. Hiyo ni sumu mbaya sana
katika mahusiano ya kimapenzi, utakuta mwanaume anataka apekuwe simu ya mke
wake lakini yeye hataki ya kwake ipekuliwe. Mwanaume akichelewa kurudi nyumbani
asiulizwe maswali lakini mwanamke akichelewa anatukanwa, huo ni uonevu mkubwa
na ni sawa kumwendesha mwenzio kama gari
wakati ni mwanadamu.
5. UBISHI.
Biblia
inawaita wanawake viumbe dhaifu kwani wanahitaji upole mwingi toka kwa wanaume,
lakini wanaume wengi hawazingatii hilo. Wanaume mwengi huonyesha upole wao
mwanzoni mwa uhusiano jambo ambalo linawafanya wanawake wengi
wadanganyike.Hatari ni kwamba upole wako utyakapoanza kupungua mwenzio anajua
humpendi na ataanza mchakato wa kuachana na wewe.Utaonyesha upole wako kwa
kusikiliza na kuheshimu maoni na hoja za mpenzi wako bila kumkatisha au
kuonyesha ukali. Pale usipomuelewa unamsikiliza ili uelewe mtazamo wake na
hisia zake na utauliza maswali kwa upole kueleweshwa mambo usiyoyajua.
6. HAONEKANI.
Mwanamke
anapenda sana mpenzi wake awe rafiki namba moja na hivyo ukaribu wake kwake ni
wa muhimu sana. Mwanaume ataonekana kuwa mbaya kwa mwanamke asipoonyesha
jitihada za kutafuta muda wa kumpigia mpenzi wake simu, kukaa nae au kucheza
nae. Mwanamke akiona moja kati ya hayo anajiona yupo hatarini na kuingiwa na
wasiwasi. Hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu mwanamke anaona hapendwi na
anaweza kukubadilikia na hutapewa sababu yake.
7. NI WA KAWAIDA.
Mwanamke
anapenda ajione kuwa mtu wa pekee sana machoni pa mpenzi wake na anatarajia
mpenzi wake awe na uwezo wa kumthibitishia hilo. Mwanaume ataonekana mbaya kwa
mwanamke pale anaposhindwa kuonyesha kuwa mpenzi wake ana utofauti mzuri zaidi
ya wanawake wengine. Hatafanya utani utani na wanawake wengine na atajivunia
mbele ya wanawake wengine kuwa ana mpenzi bora. Wengine utakuta wanaleta stori
za wapenzi wao wa zamani au kuwa na mawasiliano na wapenzi wao wa zamani jambo
ambalo linawaumiza wanawake wengi.Utaonekana wa kawaida katika uvaaji wako,
maongezi yasionoga na kuwa mchoyo kwake.
8. HANA STORI.
Tafiti
zinaonyesha kuwa wanawake wanapendelea sana stori na maongezi yanayonoga.
Wanasayansi wanajua kuwa kutokana na ukweli huo wanawake ni wepesi wa kujifunza
kuongea lugha ya kigeni kuliko wanaume, na pia watoto wa kike ndio wanaopata
uwezo wa kuongea mapema zaidi ya wavulana. Mwanaume ataonekana hafai kwa
mwanamke iwapo atakuwa hana uwezo wa kuanzisha mazungumzo matamu au mjadala
mtamu. Hata mwanaume awe amekamilika vipi katika idara nyingine zote
akipungukiwa eneo hili la maongezi yanayonoga ataonekana anaboa kwa mwanamke
alie nae.
9. HAJUI KUCHEZA NGOMA YA WAKUBWA.
Ukitaka kujua
ngoma ya wakubwa ni muhimu sana kwa mwanamke fikiria jambo lifuatalo. Je,
mwanaume ambaye hajatahiriwa atakubaliwa na kupendwa na mwanamke katika
ulimwengu wa leo? Wanawake wengi wakikutana na mwanaume ambae hajatahiriwa ni
sawa na muislamu kukutana na nguruwe msikitini, hivyo haikubaliki. Kutokana na
matatizo ya nguvu za kiume, tatizo la kuwahi kumaliza, maumbile madogo na
ujinga wa kutojua maeneo 14 yalio muhimu katika mwili wa mwanamke wanaume wengi
wameonekana vimeo kwa wake zao. Asilimia 93 ya wateja wangu ni wanaume na
ninashuhudia katika hao ni asilimia 10 tu ambao watakuja ofisini kwangu kwa
kuleta shida ya kutoelewana na mpenzi au mke. Wanaume wengi aidha wanaliona ni
tatizo la kawaida kwao au wanadharau wanawake na kuwaona kuwa hawana haki ya
kufurahia kucheza ngoma ya wakubwa. Mwanaume yeyote anaefanya kosa hilo ni
mbaya kwa mwanamke yeyote yule.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni