Jumatano, 1 Novemba 2017

SABABU ZA MWANAUME KUACHWANA MWANAMKE

        Napata vilio vingi toka kwa wanaume ambao bado wanawapenda wapenzi wao au wake zao lakini watu hao wamebadilika na kuwafanyia mambo yanayowaumiza mno. Upende au usipende kuna vigezo ambavyo mpenzi wako anaangalia na unaposhindwa kutimiza vigezo hivyo mwanamke ataanza kuleta misukosuko ambayo kwako wewe kama mwanaume utaona kuwa haina sababu. Hebu fikiria, umempenda mwanamke mrembo na yeye akakukubali na kuapa kuwa hatakuacha kabisa unadhani kwa maneno hayo hawezi kukuacha?
Nikupe mfano mmoja, kaka mmoja alipata mchumba ambae alikuwa mrembo sana na kwa miaka 3 uhusiano ulikuwa mtamu mpaka pale huyo kaka alipoanza matani na dada mwingine. Yeye aliona ni utani lakini baada ya mchumba wake kuona mtiririko wa mazungumzo yao kwa SMS alijua kuwa mchumba wake anao uwezo mkubwa sana wa kumsaliti. Japo alikuwa hajathibitisha kabisa alivunja uchumba huo, unaweza kupiga kelele na kusema kuwa huyo dada alikosea alitafuta tu kisingizio. Sikiliza dada ambae baba yake alichepuka na kumletea mama yake UKIMWI lazima atachukia usaliti hata chembe ndogo tu ya usaliti inamtisha sana.
Vifuatavyo ni vitu au mambo mabaya kwa wanawake:
1.  MATANGAZO YA UONGO.
        Katika miaka 11 ya utoaji ushauri katika Radio na TV nimekutana na kesi nyingi za wanaume walioachwa japo bado walikuwa wanawapenda wapenzi wao. Wanaume wengi ni mabingwa katika kutangazia wanawake kuwa wanawapenda lakini hawajui njia sahihi za kuwathibitishia hilo. Kaka mmoja alishtuka pale ambapo dada ambae alizoea kumuita “Mpenzi” au “Honey” ama “Darling” alipobadilisha hayo majina na kuanza kumuita huyo kaka “Wewe”. Nilipomuuliza huyo kaka iwapo amewahi kumpa zawadi yoyote mpenzi wake aliniambia juu ya misaada aliyoitoa kama kuharibikiwa na simu ya mpenzi wake kulimlazimisha atoe pesa itengenezwe, kumpa nauli kwenda misibani na vitu vingine. Nikamwambia hiyo sio zawadi bali ni msaada. Mwanamke hajali maneno unayotumia kumwambia unampenda bali anataka umfanyie mambo bila ya kuombwa au kuambiwa, hapo ndio anauona moyo wako wa kupenda. Ukitoa ahadi zako jitahidi uzitimize na pia jitahidi kuwa nae karibu pale upatapo nafasi.Unaposhindwa kuwa mtu wa vitendo unaonekana kuwa  unacheza mchezo wa kuigiza tu.

2.  KUHAMIA KITI CHA NYUMA.
        Wanaume wengi sana huonyesha msisimko wao mwanzoni mwa uhusiano na hawaweki mikakati ya kudumisha shangwe hizo. Baada ya muda fulani uchangamfu uliokuwepo mwanzoni unapungua na mawasiliano yanakuwa madogo. Mwanzoni wanaume wanakuwa wawazi kwa wapenzi wao lakini baadae wanaanza usirisiri na hawataki kuulizwa maswali na wakiulizwa wanakuwa wakali. Utaonekana mbaya kwa mwanamke pale unapomtegea kuwa yeye ndio awe wa kwanza kukutafuta ,kukupa zawadi na akakubali kila unapotaka kucheza nae ngoma ya wakubwa. Kufanya hivyo ni sawa na abiria aliekuwa amekaa kiti cha mbele ndani ya gari na anahamia kiti cha nyuma. Kwa kuwa mwanamke anakuwa hajapata sababu za kutosha kwa mabadiliko hayo anajua kuwa umemchoka.

3.  KUJIFANYA KIPOFU NA KIZIWI.
        Wanaume wengi hawajajifunza kuwa makini katika mahusiano yao jambo ambalo linawaboa wanawake. Mwanaume hamsifii uzuri wa mpenzi wake, uvaaji wake na bidii yake katika usafi, anakuwa kama vile kipofu ambaye haoni hayo yote. Hata Mungu alilalamika juu ya mambo yanayofanana na hayo: “Sikilizeni enyi viziwi; tazameni enyi vipofu, mpate kuona. Ni nani alie kipofu kama mtumishi wangu, au alie kiziwi kama mjumbe wangu nimtumaye? Unaona mambo mengi lakini huyatii moyoni, masikio yako yapo wazi lakini husikii” (ISAYA 42: 19-20).
Ni muhimu mwanaume ajifunze kumsifia mpenzi wake na kumshukuru kwa mambo anayofanyiwa. Mwanaume mbaya haoni umuhimu wa kumtamkia mpenzi wake mara kwa mara kama anampenda.

4.  UDEREVA.
        Asilimia kubwa ya wanaume wanapata shida kuelewa kuwa mwanamke nae ni mwanadamu mwenye akili anaehitaji kusikilizwa. Utakuta mwanaume anataka mambo yaende kama anavyotaka yeye bila kujali hisia za mwanamke. Na sio hilo tu, bali pia wanaume wengi wabaya sio wepesi kwa kukubali kosa au kuomba radhi. Hiyo ni sumu mbaya sana katika mahusiano ya kimapenzi, utakuta mwanaume anataka apekuwe simu ya mke wake lakini yeye hataki ya kwake ipekuliwe. Mwanaume akichelewa kurudi nyumbani asiulizwe maswali lakini mwanamke akichelewa anatukanwa, huo ni uonevu mkubwa na ni sawa  kumwendesha mwenzio kama gari wakati ni mwanadamu.

5.  UBISHI.
        Biblia inawaita wanawake viumbe dhaifu kwani wanahitaji upole mwingi toka kwa wanaume, lakini wanaume wengi hawazingatii hilo. Wanaume mwengi huonyesha upole wao mwanzoni mwa uhusiano jambo ambalo linawafanya wanawake wengi wadanganyike.Hatari ni kwamba upole wako utyakapoanza kupungua mwenzio anajua humpendi na ataanza mchakato wa kuachana na wewe.Utaonyesha upole wako kwa kusikiliza na kuheshimu maoni na hoja za mpenzi wako bila kumkatisha au kuonyesha ukali. Pale usipomuelewa unamsikiliza ili uelewe mtazamo wake na hisia zake na utauliza maswali kwa upole kueleweshwa mambo usiyoyajua.

6.  HAONEKANI.
        Mwanamke anapenda sana mpenzi wake awe rafiki namba moja na hivyo ukaribu wake kwake ni wa muhimu sana. Mwanaume ataonekana kuwa mbaya kwa mwanamke asipoonyesha jitihada za kutafuta muda wa kumpigia mpenzi wake simu, kukaa nae au kucheza nae. Mwanamke akiona moja kati ya hayo anajiona yupo hatarini na kuingiwa na wasiwasi. Hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu mwanamke anaona hapendwi na anaweza kukubadilikia na hutapewa sababu yake.

7.  NI WA KAWAIDA.
        Mwanamke anapenda ajione kuwa mtu wa pekee sana machoni pa mpenzi wake na anatarajia mpenzi wake awe na uwezo wa kumthibitishia hilo. Mwanaume ataonekana mbaya kwa mwanamke pale anaposhindwa kuonyesha kuwa mpenzi wake ana utofauti mzuri zaidi ya wanawake wengine. Hatafanya utani utani na wanawake wengine na atajivunia mbele ya wanawake wengine kuwa ana mpenzi bora. Wengine utakuta wanaleta stori za wapenzi wao wa zamani au kuwa na mawasiliano na wapenzi wao wa zamani jambo ambalo linawaumiza wanawake wengi.Utaonekana wa kawaida katika uvaaji wako, maongezi yasionoga na kuwa mchoyo kwake.

8.  HANA STORI.
        Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanapendelea sana stori na maongezi yanayonoga. Wanasayansi wanajua kuwa kutokana na ukweli huo wanawake ni wepesi wa kujifunza kuongea lugha ya kigeni kuliko wanaume, na pia watoto wa kike ndio wanaopata uwezo wa kuongea mapema zaidi ya wavulana. Mwanaume ataonekana hafai kwa mwanamke iwapo atakuwa hana uwezo wa kuanzisha mazungumzo matamu au mjadala mtamu. Hata mwanaume awe amekamilika vipi katika idara nyingine zote akipungukiwa eneo hili la maongezi yanayonoga ataonekana anaboa kwa mwanamke alie nae.

9.  HAJUI KUCHEZA NGOMA YA WAKUBWA.
        Ukitaka kujua ngoma ya wakubwa ni muhimu sana kwa mwanamke fikiria jambo lifuatalo. Je, mwanaume ambaye hajatahiriwa atakubaliwa na kupendwa na mwanamke katika ulimwengu wa leo? Wanawake wengi wakikutana na mwanaume ambae hajatahiriwa ni sawa na muislamu kukutana na nguruwe msikitini, hivyo haikubaliki. Kutokana na matatizo ya nguvu za kiume, tatizo la kuwahi kumaliza, maumbile madogo na ujinga wa kutojua maeneo 14 yalio muhimu katika mwili wa mwanamke wanaume wengi wameonekana vimeo kwa wake zao. Asilimia 93 ya wateja wangu ni wanaume na ninashuhudia katika hao ni asilimia 10 tu ambao watakuja ofisini kwangu kwa kuleta shida ya kutoelewana na mpenzi au mke. Wanaume wengi aidha wanaliona ni tatizo la kawaida kwao au wanadharau wanawake na kuwaona kuwa hawana haki ya kufurahia kucheza ngoma ya wakubwa. Mwanaume yeyote anaefanya kosa hilo ni mbaya kwa mwanamke yeyote yule.   
     

Maoni 1 :

                                    HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE  Mwanamke anapojikuta amepoteza hamu ya tendo la ndoa anakuwa mzigo k...